#46
Twae wangu uzima
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku, Zikutukuze huku.
Couplet 2
Twae mikono nayo Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu Kwa wongozi wako tu.
Couplet 3
Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako.
Couplet 4
Twae dhanabu pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.
Couplet 5
Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako.
Couplet 6
Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi Nniwe wako halisi.