#45
Mtazame Huyo aliyeangikwa juu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu Wala usifanye tashwishi.
Refrain
Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.
Couplet 2
Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi, Na makosa yako maovu! Kama deni zetu zote hakulipa Mbona imemwagika damu?
Refrain
Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.
Couplet 3
Si kutubu na sala ikomboayo, Ila damu ndiyo salama; Na aliyeimwaga aweza, sasa, Dhambi zako kukufutia.
Refrain
Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.
Couplet 4
Usiwe na shaka, Mungu amesema, Hakuna alilolisaza; Hapo alipokuja alitimiza Kazi zote alizoanza.
Refrain
Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.
Couplet 5
Basi twae uzima, kwa kufurahi Upokee kwa Bwana, sasa; Ujijue hakika kwake kuishi Yesu aishiye kabisa.