Indirimbo Zikundwa Open in the app

#41

Yesu aliniita, “Njoo”

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu aliniita, “njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze Kifuani mwangu.” Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka; Nikapata kwake raha, Na furaha tena.

Couplet 2

Yesu aliniita, “njoo, Kwangu kuna maji, Maji ya uzima, bure, Unywe uwe hai, ” Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa: Naishi kwake, na kiu Kamwe sina tena.

Couplet 3

Yesu aliniita, “njoo, Dunia ni giza, Ukinitazama nuru Takung’arizia.” Nilikwenda kwake mara Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga Safarini mwangu.