#40
Nasikia Kuitwa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Nasikia kwitwa Na sauti yako Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.
Refrain
Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
Couplet 2
Ni mnuonge kweli, Umenipa nguvu, Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu.
Refrain
Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
Couplet 3
Yesu hunijuvya; Mapenzi, imani; Tumai, amani, radhi, Hapa na Mbinguni.
Refrain
Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
Couplet 4
Huipa imara, Kazi yake, ndani: Huongezeka neema, Ashindwe Shetani.
Refrain
Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
Couplet 5
Huishuhudia, Myoyo ya imani Ya kuzipata ahadi, Wakimuamini.
Refrain
Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
Couplet 6
Napata Wokovu, Wema na neema; kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.