#39
Mwenye dhambi huna raha
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mwenye dhambi huna raha, Sikiza nakusihi, Utapata msamaha Kwake Yesu Mwokozi! Njoo hima, njoo hima, Naye atafurahi.
Couplet 2
Yesu anakwita sana Naye yuko Mbinguni; Hofu ya kifo hapana Kwake ukiamini. Njoo hima, njoo hima, Utapata amani.
Couplet 3
Hatakwita siku zote; Ni ya sasa nafasi. Lete na uchafu wote, Kukawa haipasi. Njoo hima, njoo hima, Ni Wokovu halisi.
Couplet 4
Uzima uko kwa Bwana Twae uzima hasa Bure unapatikana, Wokovu twae sasa! Njoo hima, njoo hima, Twae utakatifu.