#38
Twende kwa Yesu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue Imo Chuoni; na Mwenyewe, Hapa asema, Njoo!
Refrain
Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa.
Couplet 2
”Wana na waje”, atwambia, Furahini mkisikia, Ndiye mfalme wetu pia, Na tumtii, Njoo.
Refrain
Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa.
Couplet 3
Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikiwapo, Ewe kijana, Njoo.
Refrain
Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa.