Indirimbo Zikundwa Open in the app

#37

Waitwa, mwovu, na Bwana

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Waitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako?

Refrain

Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni.

Couplet 2

Alilipa damu yake Ili kukukweza kwake; Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema.

Refrain

Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni.

Couplet 3

Ukifanywa kuwa mwema Mwishoni utasimama, Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani.

Refrain

Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni.

Couplet 4

Ni mwanga tu, nchi ile; Uovu hauko kule, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke.