Indirimbo Zikundwa Open in the app

#33

Dhambi ikikulemea

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Dhambi ikikulemea, Kwa Bwana rehema; Hivi sasa tegemea Neno la salama.

Refrain

Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.

Couplet 2

Yesu amemwaga damu Ya nyingi baraka; Nawe sasa oga mumu Zioshwamo taka.

Refrain

Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.

Couplet 3

Ni njia yeye hakika Hwongoza rahani; Usikawe kumshika, Uwe barakani.

Refrain

Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.

Couplet 4

Karibu nawe wingie Mwetu safarini, Twende tukamwamkie, Milele Mbinguni.

Refrain

Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.