Indirimbo Zikundwa Open in the app

#32

Yesu awakubali wakosa

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu awakubali, Wakosa, wahalifu, Wambieni wa mbali Habari ya Wokovu.

Refrain

Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!”

Couplet 2

Awakubali Bwana Neno lake amini Watu kila aina Waje kwake tengoni.

Refrain

Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!”

Couplet 3

Mimi ni safi moyo Na mbele ya sharia, Aliye safi roho Kwake ilitimia.

Refrain

Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!”

Couplet 4

Akubali wakosa; Nami anikubali; Alivyonitakasa Mbinguni niwasili.