#34
Njoni! Wenye dhambi
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu awangojea ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye kuwaponya ni Yeye.
Couplet 2
Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha, Imani, kweli, na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, kwake Bwana Bure utapata.
Couplet 3
Njoni, mliolemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu.
Couplet 4
Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha alipoangikwa Akalia mtini; ” Imekwisha”, alitosha Dhabihu ya thamani.
Couplet 5
Kristo aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai yeye; Kamwe mwingine hako Yesu pweke, Yesu pweke, Ndiye Mwokozi wako.
Couplet 6
Wamsifu-sifu sana Mbinguni malaika; Wachanganya nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya wataimba Waliooshwa taka.