#31
Msingi imara
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili; Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia.
Couplet 2
Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takupa nawe, nikuwezeshe, Ipata kufaa, isikutishe!
Couplet 3
Utakapopishwa ndani ya moto Nnguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako.
Couplet 4
Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo.
Couplet 5
Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanam zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha.