#30
Nilikuwa Kondoo aliyepotea
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda baba yangu wala kutulia.
Couplet 2
Na Mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa.
Couplet 3
Yesu ni Mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.
Couplet 4
Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na Mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.