#29
Baba Yetu aliye Mbinguni
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Baba yetu aliye Mbinguni Amenifurahisha yakini Kuniambia mwake chuoni Ya kuwa nami Yesu pendoni.
Refrain
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.
Couplet 2
Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli, Hunirejeza kwake moyoni; Kweli yu nami Yesu pendoni.
Refrain
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.
Couplet 3
Anipenda! Nami nampenda; Kwa Wokovu alionitenda; Akanifia Msalabani Kwa kuwa nami Yesu pendoni.
Refrain
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.
Couplet 4
Haya kujua yanipa raha; Kumuamini kuna furaha; Humfukuza mara Shetani, Kwona yu nami Yesu Pendoni.
Refrain
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.
Couplet 5
Sifa ni nyingi asifiwazo, Moja ni sana katika hizo, Wala siachi, hata Mbinguni, Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.