#26
Yesu unipendaye
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; Nifiikishe Mbinguni Wokoe moyo wangu.
Couplet 2
Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana , Nipe neema yako, Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha.
Couplet 3
Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, Uongoze vipofu.
Couplet 4
Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima.