Indirimbo Zikundwa Open in the app

#25

Nimekombolewa na Yesu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake.

Refrain

Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.

Couplet 2

Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake.

Refrain

Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.

Couplet 3

Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake.

Refrain

Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.

Couplet 4

Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo.

Refrain

Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.