Indirimbo Zikundwa Open in the app

#24

Mwokozi moyoni mwangu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni mwangu, Sina giza tena, ila mwanga pia Kwa Yesu Mwokozi wangu.

Refrain

Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.

Couplet 2

Sina haja tena, ya kutanga-tanga, Ndiye kiongozi wangu. Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu, Mwanawe Mungu.

Refrain

Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.

Couplet 3

Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu zimeondoka, kwa kuwa ninaye Yesu.

Refrain

Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.

Couplet 4

Siogopi tena, nikiitwa kufa, Yu nami daima, Yesu. Mlango wa Mbinguni ni yeye pia, “Tapita humo kwa damu.”

Refrain

Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.

Couplet 5

Nitaketi na yeye huko milele, Nisifu Mwokozi wangu. Nina raha moyoni majira.