Indirimbo Zikundwa Open in the app

#23

Ni salama rohoni mwangu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 2

Ingawa Shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.

Refrain

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 3

Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa Msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 4

Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.