#22
Kale nilitembea
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Kale nilitembea Nikilemewa dhambi Nilikosa msaada, kuniponya mateso.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 2
Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba, Palinifaa sana, Sitasahau kamwe.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 3
Hicho ndicho chanzo, Cha kufurahi kwangu. Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 4
Panapo Msalaba, Kinatolewa cheti, Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 5
Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti, Kitumai kwingia, Kama walio nacho.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 6
Lipofika langoni, Akaulizwa cheti, Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 7
Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho, Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 8
Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu, Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho.
Refrain
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Couplet 9
Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi, Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako.