Indirimbo Zikundwa Open in the app

#21

Roho yangu hima

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Roho yangu hima, na taa yako Kaiwashe vyema, hapa si pako; Nguvu zote pia za duniani Hazitakudhuru ukiamini.

Refrain

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

Couplet 2

Adui Shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; Wewe nguvu huna, huna kabisa, Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.

Refrain

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

Couplet 3

Toka na mapema, mbele ya wote, Omba, bisha sana, maisha yote; Vita vikaliko, macho ukae, Jivike silaha, nawe sishindwe.

Refrain

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

Couplet 4

Bwana Yesu ndiye kwako Mchunga, Neno lake Bwana ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, Neno lake Bwana laendelea.

Refrain

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.