Indirimbo Zikundwa Open in the app

#20

Ninaye rafiki naye

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ninaye Rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo zake Nimefungwa milele; Aukaza moyo wangu, Uache mageule, Mimi wake, yeye wangu; Ndimi naye milele.

Couplet 2

Ninaye rafiki ndiye Aliyenifilia; Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia; Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele; Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.

Couplet 3

Ninaye rafiki naye Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu tachukuliwa; Nikitazama Mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele.

Couplet 4

Ninaye rafiki naye, Anao moyo mwema; Ni mwalimu, kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga Na mapenzi ya mbele? Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.