#19
Ndiyo Dhamana Yesu wangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ndiyo dhamana, Yesu wangu; Hunipa furaha za Mbingu; Mrithi wa Wokovu wake Nimezawa kwa Roho yake.
Refrain
Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu.
Couplet 2
Kumsalimu moyo wangu, Mara namwona raha yangu; Aniletea malaika, Wananilinda, taokoka.
Refrain
Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu.
Couplet 3
Sina Kinyume, nashukuru, Mchana kutwa huja kwangu; Usiku kucha kuna nuru; Mwokozi wangu; ndimi huru.
Refrain
Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu.
Couplet 4
Hali na mali anitwaa! Mara namwona anifaa, Nami nangoja kwa subira; Akiniita, nije mara.