#18
Akifa Yesu Nikafa naye
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Akifa Yesu nikafa naye Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka aje: Nyakati zote ni wake yeye.
Refrain
Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.
Couplet 2
Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki.
Refrain
Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.
Couplet 3
Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali.
Refrain
Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.
Couplet 4
Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila kitini Daima hunifikiri mimi.
Refrain
Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.
Couplet 5
Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia.