#17
Namwandama Bwana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Namwandama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia.
Refrain
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
Couplet 2
Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.
Refrain
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
Couplet 3
Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki Taamini nitii pia.
Refrain
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
Couplet 4
Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia.
Refrain
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
Couplet 5
Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda, nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia.
Refrain
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.