Indirimbo Zikundwa Open in the app

#14

Yesu kwa imani

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo.

Couplet 2

Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu.

Couplet 3

Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata.

Couplet 4

Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo name Nami nikwandame Siku zote.