#13
Tafuta daima utakatifu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Tafuta daima utakatifu; Fanya urafiki na WaKristo tu; Nena siku zotena Bwana wako, Baraka uombe kwa kila jambo.
Couplet 2
Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia Mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo.
Couplet 3
Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako aew Yesu tu; Katika furaha au huzuni Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.
Couplet 4
Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako; Akikuongoza katika haki, Hufanywa tayari kwa kazi yake.