Indirimbo Zikundwa Open in the app

#12

Ewe Roho wa Mbinguni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya Kanisa.

Couplet 2

Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana.

Couplet 3

Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote.

Couplet 4

Ndiwe Umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye Baraka.

Couplet 5

Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na kichwa Mbinguni.