Indirimbo Zikundwa Open in the app

#8

Taji mvikeni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Taji mvikeni, Taji nyingi tena, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana; Name tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Mkuu wa Mbingu.

Couplet 2

Taji mvikeni Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani Aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu vya Yese, Wa Bethirehemu.

Couplet 3

Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna Hata malaika Awezaye kuziona Pasipo kushangaa.