#7
Ni tabibu wa karibu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ni tabibu wa karibu; Tabibu wa ajabu; Na rehema za daima; Ni dawa yake njema.
Refrain
Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.
Couplet 2
Hatufai kuwa hai, Wala hatutumai, Ila kweli yeye ndiye Atupumzishaye.
Refrain
Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.
Couplet 3
Dhambi pia na hatia Ametuchukulia; Twendeni na amani Hata kwake Mbinguni.
Refrain
Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.
Couplet 4
Huliona tamu jina La Yesu Kristo Bwana, Yuna sifa mwenye kufa Asishindwe na kufa.
Refrain
Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.
Couplet 5
Kila mume asimame, Sifa zake zivume; Wanawake na washike Kusifu jina lake.
Refrain
Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.
Couplet 6
Na vijana wote tena, Wapendao sana Waje kwake wawe wake Kwa utumishi wake.