Indirimbo Zikundwa Open in the app

#9

Yesu kwetu ni Rafiki

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu kwetu ni Rafiki, Hwamiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia; Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya; Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia.

Couplet 2

Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia. Haifai kufa moyo, Dua atasikia Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; Maombi asikia.

Couplet 3

Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea, Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau, Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia.