Indirimbo Zikundwa Open in the app

#173

Bwana Yesu, Uniongoze

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Bwana Yesu, Uniongoze kwa bahari ya maisha, Hata kwa mawimbi mengi, kwa zoruba ya hatari; Bwana Yesu, uniongoze, nakutegemea wewe.

Couplet 2

Bwana Yesu, uniongoze, utulize moyo wangu; Neno moja toka kwako lilinyamazisha pepo. Bwana Yesu, uniongoze, leta utulivu wako.

Couplet 3

Bwana Yesu, uniongoze, niyashinde majaribu; Mengi yananidanganya, mengi yanafunga macho; Bwana Yesu, uniongoze, niwe mushindaji kweli.

Couplet 4

Bwana Yesu, uniongoze, nitakapovuka ngambo; Nikiona woga, giza, leta nuru na amani; Bwana Yesu, uniongoze, uwe nami hata mwisho.