#172
Sina woga kwenda na Mwokozi Yesu
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Sina woga kwenda na Mwokozi Yesu, Ataniongoza na kunibariki; Bila Yesu sitakuwa na furaha. Yesu tu anafukuza woga wote.
Refrain
Kila pa’li na Mwokozi sitajua woga, Kila pa’li na Mwokozi nitakwenda.
Couplet 2
Na Mwokozi sitakuwa peke yangu, Hata nikiashwa na rafiki zangu; Hata akiniongoza kwa mateso, Nitasifu kwani Yesu ni karibu.
Refrain
Kila pa’li na Mwokozi sitajua woga, Kila pa’li na Mwokozi nitakwenda.
Couplet 3
Kili pa’li Yesu anaponituma Kutangaza Neno lake la Wokovu, Nitapenda kwenda kama akiita, Ao kubaki hapa kama akitaka.
Refrain
Kila pa’li na Mwokozi sitajua woga, Kila pa’li na Mwokozi nitakwenda.
Couplet 4
Yesu ni pamoja nami, nitalala Saa ya giza la usiku bila woga, Nikijua kwake Mbingu nitafika Na safari hapa itamalizika.
Refrain
Kila pa’li na Mwokozi sitajua woga, Kila pa’li na Mwokozi nitakwenda.