Indirimbo Zikundwa Open in the app

#137

Tamu sana ni Maneno ya Habari njema

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Tamu sana ni Maneno ya Habari njema, Jana, leo, na milele Yesu yuko sawa; Hata sasa anapenda watu wa makosa, Kufariji wenye taabu, sifu Jina lake.

Refrain

Jana, leo, na milele Yesu yuko sawa, Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa. Sifu Jina lake Sifu Jina lake Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa.

Couplet 2

Mwenye kusamehe Petro atatusamehe; Atatoa shaka zote kama kwa Tomasi; Mwanafunzi alilala kifuani mwake; Anaita watu sasa kupumzika kwake.

Refrain

Jana, leo, na milele Yesu yuko sawa, Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa. Sifu Jina lake Sifu Jina lake Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa.

Couplet 3

Alinyamazisha maji kule kwa bahari, Hivyo anaweza kuondoa woga vile; Akaomba na huzuni kwa Getesemane; Anaweza kufahamu taabu zetu zote

Refrain

Jana, leo, na milele Yesu yuko sawa, Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa. Sifu Jina lake Sifu Jina lake Vyote vinapogeuka, Yesu yuko sawa.

Couplet 4

Kama alivyotembea na wafuasi wake, Na kuwafariji kwa safari ya Emau, Vivyo hivyo anapenda kutembea nasi Yeye Mufariji mwema leo na milele