#136
Nina Mwokozi Anayeniombea
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Nina Mwokozi Anayeniombea, Rafiki kuliko wengine wo wote; Na sasa Mbinguni ananitunza sana, Laiti upate Mwokozi mwenyewe.
Refrain
Ninakuombea, ninakuombea, Ninakuombea, upate kuamini.
Couplet 2
Nina taraja kutoka Baba wangu, Ya kama atanipokea Mbinguni; Na sasa ninamungojea kuniita, Laiti upate taraja yenyewe.
Refrain
Ninakuombea, ninakuombea, Ninakuombea, upate kuamini.
Couplet 3
Nina mavazi yanayoningojea, Mavazi meupe ndiyo utukufu; Na nitayapata Mbinguni kwake Mungu, Laiti upate mavazi yenyewe.
Refrain
Ninakuombea, ninakuombea, Ninakuombea, upate kuamini.
Couplet 4
Nina salama inayopita yote, Si kama dunia inayoitoa; Inatoka Yesu kwa Pendo lake kubwa, Laiti upate salama yenyewe.
Refrain
Ninakuombea, ninakuombea, Ninakuombea, upate kuamini.