Indirimbo Zikundwa Open in the app

#87

Yote ninayo niliyapokea

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yote ninayo niliyapokea Kwa wema wake unaoenea; Mimi si kitu, namutegemea; Nimeokolewa kwa Neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, Kwa Pendo lake nimeokoka Yesu ni Mwema na mwenye Rehema. Nimeokolewa kwa Neema.

Couplet 2

Nilitembea zamani kwa zambi Katika njia ya kufa, lakini Yesu alinitafuta polini; Nimeokolewa kwa Neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, Kwa Pendo lake nimeokoka Yesu ni Mwema na mwenye Rehema. Nimeokolewa kwa Neema.

Couplet 3

Nimetakaswa na Yesu Mwokozi, Si kwa matendo na si kwa machozi, Ila kwa damu nina ukombozi; Nimeokolewa kwa Neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, Kwa Pendo lake nimeokoka Yesu ni Mwema na mwenye Rehema. Nimeokolewa kwa Neema.

Couplet 4

Raha ya Mbingu imeniingia, Kwa shangwe kubwa namufurahia. Kwa kuwa Yesu ‘nanirehemia; Nimeokolewa kwa Neema.