#86
Neema ya Bwana ni kubwa sana
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Neema ya Bwana ni kubwa sana, Kubwa kuliko zambi za watu, Kule Kalvari tunaiona, Pa’li pa kufa kwa Bwana Yesu.
Refrain
Neema yake inasamehe makosa yetu, Neema yake kubwa kuliko uovu wetu.
Couplet 2
Tuko katika hatari kubwa, Tutapotea tusipotubu; Neema ya Bwana inaonyesha Yesu Mwokozi ni kimbilio.
Refrain
Neema yake inasamehe makosa yetu, Neema yake kubwa kuliko uovu wetu.
Couplet 3
Ndugu, huwezi kuficha zambi, Mungu Mbinguni anaziona Ee unataka kusukuliwa? Damu ya Yesu itakuosha.
Refrain
Neema yake inasamehe makosa yetu, Neema yake kubwa kuliko uovu wetu.
Couplet 4
Neema ya Bwana ni kubwa sana, Iko tayari kwawe, Mupenzi; Kiri makosa, amini Yesu. Atasamehe kwa Neema yake.
Refrain
Neema yake inasamehe makosa yetu, Neema yake kubwa kuliko uovu wetu.