#43
Bwana unirehemu
Impimbano
Couplet 1
Mimi mwenye dhambi ningekufa; lakini wewe Bwana wangu ukazichukua; Yesu ulikubali kuchubuliwa ili mimi mwenye dhambi niokolewe.
Refrain
{Bwana nakuomba unirehemu; nifuate nyayo zako milele.} x2
Couplet 2
Pale Golgota Yesu Bwana wangu; ukasema leo yote yamekwisha; niliwekwa huru na damu yako; nilinunuliwa kwa thamani nyingi.
Refrain
{Bwana nakuomba unirehemu; nifuate nyayo zako milele.} x2
Couplet 3
Wateule wako tunangojea; ahadi zako zitatimizwa; mvua itanyesha na tutanyakuliwa; Mbingu tutaishi hata kutawala.
Refrain
{Bwana nakuomba unirehemu; nifuate nyayo zako milele.} x2
Couplet 4
Katika safari wengi walikufa; wengi majeraha na kurudi nyuma; njia ni nyembamba tunakazana kwa neema yako tutamaliza
Refrain
{Bwana nakuomba unirehemu; nifuate nyayo zako milele.} x2
Couplet 5
Mateso na shida tutavisahau hata na machozi yetu utapangusa; tutashangilia tutafurahia wewe Bwana-Arusi tukikulaki.
Refrain
{Bwana nakuomba unirehemu; nifuate nyayo zako milele.} x2