Indirimbo Zikundwa Open in the app

#290

Zamani tulikuwa

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Zamani tulikuwa katikati ya giza, Sasa tumeona nuru ni Bwana; Na tena tulikuwa mu kivuli cha kufa, Tumepewa nuru, si’ mataifa.

Refrain

Utawala wa Mwokozi (Salama, milele, milele!) Hautakuwa na mwisho, (Furaha, salama, milele!) Sifa Mbingu na dunia! (x2) (yote)

Couplet 2

Ume’ngoza taifa, umezidisha furaha, Asante kwa Mungu Baba wa vyote; Tunafurahi sana mbele yako, ee Bwana, Furaha kama siku ya mavuno.

Refrain

Utawala wa Mwokozi (Salama, milele, milele!) Hautakuwa na mwisho, (Furaha, salama, milele!) Sifa Mbingu na dunia! (x2) (yote)

Couplet 3

Kwa mana’mevunja nira la muzigo wake Na gongo la bega lake, ee Bwana; Na fimbo lake yeye aliyemuonea, Kama katika siku ya Midiani.

Refrain

Utawala wa Mwokozi (Salama, milele, milele!) Hautakuwa na mwisho, (Furaha, salama, milele!) Sifa Mbingu na dunia! (x2) (yote)

Couplet 4

Utawala’takuwa yulu ya Bega Lake, Jina litaitwa: Mwenye Ajabu; Ye’ ni Mwenye Shauri, Mungu Mwenye Uwezo, Baba wa milele na wa Salama.