Indirimbo Zikundwa Open in the app

#328

Bwana Yesu ’tuongoze wende mbele

Wokovu

Couplet 1

Bwana Yesu ’tuongoze, wende mbele yetu. Sisi tuwe nyuma yako, tufike Sayuni. Sisi peke hatuwezi kuongoza njia yetu. Ulisema peke yako, wewe ndiwe njia.

Couplet 2

Huku chini duniani tunahangaishwa. Vinavyotuhangaisha vitabaki huku. Bwana Yesu tunachoka, tuwezeshe safarini. Kwa kungoja baragumu tushushie Roho.

Couplet 3

Mambo mengi yanafichwa kwa kukosa Moto. Watu wengi wanacheza na maovu yao. Wanadhani huwaoni, mwovu anawadanganya. Tuma uamsho, Bwana, urudishe wengi.

Couplet 4

Twakwambia leo, ndugu, usidanganyike. Bwana Yesu anajua njia zako zote. Hata ikiwa usiku kwake kuna nuru wazi. Acha njia zile ndugu, saa zingaliko.

Couplet 5

Usidhani hakuoni, anavumilia. Anangoja siku ile atimize yote. Una heri leo, ndugu, kwani tunakukumbusha. Fika leo kwa Mwokozi, saa zinapita.

Couplet 6

Anabisha mlangoni, umfungulie, anataka aingie kuokoa wewe. Mbona humfungulie? Anakuhitaji wewe. Ne’ma kwako itakwisha, utahukumiwa.

Couplet 7

Una heri, ndugu, wewe uliye hokoka, Bwana Yesu akirudi, tutashangilia. Tutamfanana Yesu, na kurithi mji ule, wa milele na milele, mji wa heri...