Indirimbo Zikundwa Open in the app

#307

Walikombolewa waimba juu

Wokovu

Couplet 1

Walikombolewa waimba juu, wakisujudu mbele zake Bwana. Huzuni na taabu zake dunia Bwana amewaondolea zote.

Refrain

Wanamwimbia Mwana Kondoo Aliyekufa, sasa yu Hai, Ameyashinda mauti.

Couplet 2

Wanashika vinubi mikononi wakiimba wimbo wa Mwana Kondoo na Musa mtumishi wake Mungu, wakifurahia kushinda kwake.

Refrain

Wanamwimbia Mwana Kondoo Aliyekufa, sasa yu Hai, Ameyashinda mauti.

Couplet 3

Wasiopenda kumsujudia, katika dunia hii ya sasa. Hawataonekana mbele zake, watateketea Motoni kweli.

Refrain

Wanamwimbia Mwana Kondoo Aliyekufa, sasa yu Hai, Ameyashinda mauti.

Couplet 4

Mda unaobaki ni mfupi, tujitayarisheni ndugu sasa. Bwana ajapo tuwepo tayari, tutaimba naye kule Mbinguni.

Refrain

Wanamwimbia Mwana Kondoo Aliyekufa, sasa yu Hai, Ameyashinda mauti.