#270
Simama fanya vita pamoja na Mfalme
Wokovu
Couplet 1
Simama, fanya vita pamoja na Mfalme! Bendera tuishike iliyo ya Mwokozi! Mwenyezi huongoza majeshi yake huku. Adui wote pia washindwa mbele yake.
Couplet 2
Sikia baragumu, linatuita sasa! Tuendelee mbele, kusudi ni kushinda! Tusiogope kamwe hatari ya shindano, pigana na adui kwa nguvu yake Mungu!
Couplet 3
Sima, fanya vita kwa jina lake Yesu! Hatuna nguvu sisi, tunamtegemea. Na kwanza tuzivae silaha zake Mungu! Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidii!
Couplet 4
Shindano letu hapa ’takwisha siku moja; twapiga vita leo, baada pumziko. Na kila mshindaji atapokea taji, na utukufu tele karibu na Mfalme.