Indirimbo Zikundwa Open in the app

#254

E’ roho yangu, sikiliza vema

Wokovu

Couplet 1

E’ roho yangu, sikiliza vema, wimbo wa juu unatufikia! Shangwe na raha unatuletea, amezaliwa Mkombozi wetu.

Refrain

Ahimidiwe Mungu wa Mbingu! Na duniani iwe raha na amani!

Couplet 2

Ninafurahi kwani wimbo huo tungali tunausikia huku. Na kwa upendo Mungu aita: "Mfike kwangu, nitawapa raha!"

Refrain

Ahimidiwe Mungu wa Mbingu! Na duniani iwe raha na amani!

Couplet 3

Katika nchi, mbali na karibu, sauti ya Mwokozi inavuma. Watu wa dhambi wanakuja kwake, awapokea na awaokoa.

Refrain

Ahimidiwe Mungu wa Mbingu! Na duniani iwe raha na amani!