#253
Siku ya furaha inatufikia
Wokovu
Couplet 1
Siku ya furaha inatufikia, siku nzuri katika nchi. Mungu asifiwa mbali na karibu! Malaika wanamshukuru Bwana.
Couplet 2
Huko Bethlehemu alipozaliwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, pendo la Mwenyezi likadhihirika; raha ya Mbinguni imefika kwetu!
Couplet 3
Ni karama kubwa tuliyoipewa kwa mkono wa Baba Mungu. Roho mfariji anatuongoza, atuonya njia iendayo kwake.