#242
Maisha yangu yote ni mali...
Wokovu
Couplet 1
Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Maungo, roho na akili, yeye ameyabadili. Siku zangu zote ni mali ya Mwokozi.
Refrain
Wakati wangu wote ni mali ya Mwokozi. Machoni pake ni amani, natumika kwa shukrani. Namsifu Yesu, amenihurumia!
Couplet 2
Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Naomba niwe mpendevu, nitafute wapotevu! Aliwanunua kwa Damu takatifu.
Refrain
Wakati wangu wote ni mali ya Mwokozi. Machoni pake ni amani, natumika kwa shukrani. Namsifu Yesu, amenihurumia!
Couplet 3
Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Unijalie kati’ mwendo kuongoza kwa upendo wana wapotevu, wapate kuokoka.
Refrain
Wakati wangu wote ni mali ya Mwokozi. Machoni pake ni amani, natumika kwa shukrani. Namsifu Yesu, amenihurumia!
Couplet 4
Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Nakaa miguuni pake, siku moja huko kwake inapita elfu pengine bila Yesu!