Indirimbo Zikundwa Open in the app

#241

Sitashawishiwa tena na dunia huku

Wokovu

Couplet 1

Sitashawishiwa tena na dunia huku, mema yote ni kwa Yesu, nampenda yeye. Katika safari yangu, Bwana Yesu wimbo wangu. Mbali, kwetu, kila saa namsifu Yesu.

Couplet 2

Mimi mtu heri sana, nampenda Yesu. Vyote nimempa yeye, namtumikia. Tumaini langu kuu nimeweka huko juu. Mbali, kwetu, kila saa namtumikia.

Couplet 3

Njia yote kwenda Mbingu nifuate Yesu! Nifanane naye Bwana, niwe nuru huku! Namkiri Yesu pote na katika hali zote! Mbali, kwetu, kila saa nifanane naye!