Indirimbo Zikundwa Open in the app

#225

Lo! Bendera mbele yako

Wokovu

Couplet 1

Lo! Bendera mbele yako, usihofu sasa! Usimame kwa imara kama Danieli!

Refrain

Uwe mhodari kama Danieli! Weka makusudi mema bila kuogopa!

Couplet 2

Wenye hofu hawawezi kuingia Mbingu. Tweka tu bendera yetu, endelea mbele!

Refrain

Uwe mhodari kama Danieli! Weka makusudi mema bila kuogopa!

Couplet 3

Mashujaa wa shetani wangeshindwa sana wakikuta jeshi la askari wa imani.

Refrain

Uwe mhodari kama Danieli! Weka makusudi mema bila kuogopa!

Couplet 4

Endelea kwa kushinda, Yesu ni Mfalme! Taji ya uzima utapata huko juu.

Refrain

Uwe mhodari kama Danieli! Weka makusudi mema bila kuogopa!