Indirimbo Zikundwa Open in the app

#202

Njoo kwa Yesu Mwokozi

Wokovu

Couplet 1

Njoo kwa Yesu Mwokozi, unayeteswa rohoni! Damu iliyomwagika itakuosha kabisa.

Refrain

Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.

Couplet 2

Mbona kukawa dhambini bila uzima wa Mungu? Uje upesi kwa Yesu ili upate amani!

Refrain

Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.

Couplet 3

Saa zapita upesi, hazitarudi kabisa. Bado kidogo na tena utapelekwa kuzimu.

Refrain

Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.

Couplet 4

Yesu atamchukua bibi-arusi Mbinguni, na tutaimba milele sifa za Mwana-kondoo.

Refrain

Huko karibu na Yesu, mbali ya mambo ya nchi, huru na heri rohoni nitafurahi milele!