Indirimbo Zikundwa Open in the app

#177

Nipe habari ya Yesu, uiandike...

Wokovu

Couplet 1

Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi, sifa iliyotangazwa na malaika zamani: Mungu wa ju’ atukuzwe, iwe amani duniani!

Refrain

Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi!

Couplet 2

Nipe habari ya Yesu, jinsi alivyohimili shida, jaribu na teso na umaskini na bezo (sic)! Maradhi zangu (sic) na dhambi aka’chukuwa mwenyewe, kila wakati tayari kusaidia wahitaji.

Refrain

Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi!

Couplet 3

Nipe habari ya Yesu, ya Msalaba na kufa, taja kaburi Mwambani, alipotoka Mwokozi! Pendo la Yesu ni kubwa, aliyekufa Golgotha, akafufuka hakika, namshukuru siku zote!

Refrain

Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi!