#175
Shamba la Mungu limeiva
Wokovu
Couplet 1
Shamba la Mungu limeiva, litayari sasa kuvunwa. Wavunaji mfike mbio kuyavuna mavuno yake!
Refrain
Bwana Yesu, twakuomba, uwatume watenda kazi wakusanye miganda yote kwako Yesu, Mwokozi Mwema!
Couplet 2
Uwatume mapema sana, na wengine kati’ mchana, hata saa ya magharibi uwaite wavuni wako!
Refrain
Bwana Yesu, twakuomba, uwatume watenda kazi wakusanye miganda yote kwako Yesu, Mwokozi Mwema!
Couplet 3
E’Mkristo anakuita, wende mbio, usichelewe! Macho yako uyainue kwani Yesu aja upesi!
Refrain
Bwana Yesu, twakuomba, uwatume watenda kazi wakusanye miganda yote kwako Yesu, Mwokozi Mwema!