Indirimbo Zikundwa Open in the app

#174

Pendo kubwa la Babangu linang’aa

Wokovu

Couplet 1

Pendo kubwa la Babangu linag’aa sikuzote, walakini anataka sisi tuwe nuru huku!

Refrain

Nuru yetu iangae mbele ya wenzetu huku, hata mtu ’moja moja aione njia njema!

Couplet 2

Dhambi zimetia giza huku chini duniani, walakini watu wengi wanatazamia nuru.

Refrain

Nuru yetu iangae mbele ya wenzetu huku, hata mtu ’moja moja aione njia njema!

Couplet 3

Ndugu yangu, angalia, taa yako iwe safi! Na kwa nuru waokoe wenzi waliopotea!

Refrain

Nuru yetu iangae mbele ya wenzetu huku, hata mtu ’moja moja aione njia njema!