#161
Umeshirikiana naye Yesu
Wokovu
Couplet 1
Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Una raha iliyo timilifu, umejazwa Roho yake ’takatifu?
Refrain
Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Kuna raha na starehe katika kuomba Mungu; akutia nguvu ya kushinda yote.
Couplet 2
Umepata imani ishindayo katika mashaka, shida huku chini? Umepata Neema ya kudumu inayokulinda katika hatari?
Refrain
Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Kuna raha na starehe katika kuomba Mungu; akutia nguvu ya kushinda yote.
Couplet 3
Kwake Yesu mahali pa amani, huko ndiko pa kuburudika sana; atujaza mioyo utulivu, tunakaa na raha na starehe.
Refrain
Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Kuna raha na starehe katika kuomba Mungu; akutia nguvu ya kushinda yote.
Couplet 4
Twafurahi kwa wema wake wote, twamsifu kwa ulinzi wake pia. Hata tukiudhiwa huku chini, atatufikisha kwake huko juu.